Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imewasilisha malalamiko mengine kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu – ICC, kutaka iangazie uporaji wa kimfumo wa maliasili zake, mashariki mwa nchi hiyo unaofanywa na kundi la M23 na wanajeshi wa Ulinzi wa Rwanda – RDF.

Hatua hiyo inakuwa wakati tayari ICC tayari ikiendelea kufanya uchunguzi mashariki mwa Kongo tangu 2004 ingawa haijabainika kama malalamishi hayo mapya yatabadilisha mwelekeo wa mahakama hiyo.

Wizara ya Sheria ya Kongo imesema katika taarifa yake kwamba, “Serikali ya DRC inasalia na wasiwasi mkubwa kuhusu mateso ya wakazi katika sehemu ya eneo lake iliyoathiriwa na vitendo vilivyoelezewa katika kesi hii.”

Kundi la waasi la M23 linaloongozwa na Watutsi, lilianzisha mashambulizi mapya mashariki mwa Kongo mwezi Machi mwaka jana, na kuteka miji na vijiji katika eneo linalopakana na Uganda na mapigano hayo yalipelekea zaidi ya watu milioni moja kuyakimbia makwao.

Kocha Kitayosce afunguka usajili 2023/24
West Ham Utd kuzitega Arsenal, Man Utd