Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho, watawafahamu wapinzani wao kwenye michuano hiyo hatua ya awali kesho Ijumaa (Agosti 13).

Hilo limefahamika baada ya Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ kutangaza tarehe maalum ya kupanga Droo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho itachezeshwa mjini Cairo, Misri Agosti 13.

tayari Shirikisho la soka Barani Afrika limeshataja tarehe maalum ya kuanza kwa Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho hatua ya awali, na kilichosalia ni kupanga ratiba ya michezo ya awali ya michuano hiyo.

Rasmi michuano ya ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho itaanza Septemba 11, na itafahamika kesho endapo klabu za Tanzania zitaanzia nyumbani ama ugenini katika vita ya kuwania nafasi ya kusonga mbele.

Simba SC na Young Africans zitaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, huku Azam FC na Bishara United Mara zikijipanga kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Kamwaga: Hatuchezi na Young Africans
Hisia za Edo Kumwembe: Ongezeko la Wakongo Ligi Kuu Tanzania Bara