Klabu ya DTB FC itakayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/23, inahusishwa na mpango wa kubadilishwa jina, baada ya kutumia jina lake halisi ilipokua ikishiriki madaraja ya chini.

DTB FC ambayo ilitangulia kujihakikishia kupanda Ligi Kuu ikitokea Ligi Daraja la Kwanza na baadae kuungana na Ihefu FC, pia inatajwa huenda ikahamishia maskani yake Mjini Singida ikitokea Dar es salaam.

Mapema leo Jumatatu picha za bango la klabu Singida Big Stars zilisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, na kutolewa maelezo yabayoihusisha DTB FC.

Hata hivyo hadi sasa Uongozi wa klabu ya DTB ambauo inatajwa kuwa mbioni kubadili jina haujasema lolote kuhusu uvumi huo.

Taifa Stars kuifuata Niger siku mbili kabla
Mwamnyeto afichua siri iliyotumika CCM Kirumba