Biashara zinatarajiwa kufungwa ndani ya miezi 6 kutokana na athari za virusi vya corona falme za kiarabu Dubai.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chama cha wafanyabiashara Dubai, takriban asilimia 70 ya biashara zinatarajiwa kufungwa ndani ya miezi 6 ijayo kutokana na jangaa Covid 19.

Kutokana na utafiti huo, asilimia 45 ya kampuni zilizohusishwa zimesema hazikuwa na mkakati wa kukabiliana na janga la Kimataifa, ambapo kampuni hizo zimesema zilichukua tahadhari ili kupunguza athari kwa wafanyakazi na utendaji.

Kampuni zote za safari na utalii, na zaidi ya nusu ya kampuni za hoteli, migahawa na biashara za jumla na rejareja zimesema zinatarajia kushuka kwa mauzo kwa zaidi ya asilimia 75.

Mlipuko wa ugonjwa wa  Covid 19 umekuwa na athari kubwa kiuchumi kwa kampuni ndogo na zile za kati.

Mpaka hivi sasa falme za Kiarabu zimerekodi visa 27,892, vifo 241 na waliopona ni 13,798.

Trump aagiza Magavana kufungua sehemu za Ibada
Uimara huduma za afya wapunguza 30% ya wagonjwa wa Fistula Tanzania

Comments

comments