Mshambuliaji kutoka nchini Zimbabwe na Azam FC Prince Mpumelelo Dube amesema anaendelea kuandika Rekodi kwa kuzifunga timu kubwa baada ya Jumapili (Mei 07) kuifungisha virago Simba SC kwenye hatua ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC).

Dube aliifungia Azam FC bao la ushindi na kuipeleka timu yake Fainali baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba SC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Dube ambaye ameifunga Simba SC mabao matatu msimu huu akianza na Ligi Kuu kwa kuipachika mabao mawili mzunguko wa kwanza na wa pili na juzi, alisema amehimiri presha za mashabiki wa timu hiyo ndio maana amekuwa akifunga.

“Nimeifunga Simba SC pia Young Africans. Kwangu ni Rekodi nzuri nimeingia kwenye kitabu cha washambuliaji waliowahi kuzifunga. Pia kama mchezaji nimeweka historia kwenye maisha yangu ya soka kuwahi kufanya hivyo.”

Amesema presha ya kucheza na timu hizo ambazo zina mashabiki wengi wapenda soka ni moja ya changamoto ya wachezaji wengi kushindwa kufunga mchezaji akipata nafasi na kukwamisha mpira nyavuni ni rekodi nzuri.

Manchester City yamkana Jude Bellingham
Babi aipeleka Young Africans fainali