Mshambuliaji kutoka nchini Zimbabwe na klabu ya Azam FC Prince Dube anatarajiwa kurudi uwanjani mwishoni mwa juma lijalo (Januari 17), bada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Dube aliyesajiliwa na Azam FC kutokea kikosi cha Highlanders ya nchini kwao Zimbabwe tayari ametimiza majuma sita akiwa nje ya uwanja baada ya kuvunjika mkono kwenye mchezo dhidi ya Young Africans Novemba 25 mwaka 2020.
Kabla ya kupata majeraha, Dube alikuwa amehusika kwenye mabao kumi ya Azam FC akifunga mabao sita na kuasisti mara nne na kufuatia taarifa hizo ni rasmi sasa Dube anatarajiwa kuikosa michuano ya Kombe la Mapinduzi 2021 inayoendelea ksiwani Unguja, Zanzibar.
Mkuu wa idara ya habari na mawasilino ya Azam FC Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amethibitisha taarifa za mshambuliaji huyo kutarajiwa kurejea uwanjani mwishinoni mwa juma lijalo, akwa kisiwani Zanzibar alipoambatana na kikosi cha Azam FC inachoshiriki mcihuano ya Kombe la Mapinduzi 2021.
Thabit amesema mshambulaiji huyo anaendelea vyema kwa sasa, na Januari 17 atarejea uwanjani kuanza mazoezi mepesi. Kufautia majeraha yake kupona, na sasa anajiandaa kuana mazoezi mepesi ili kurejesha utimamu wa mwili.
“Ilikua vigumu kwa Prince Dube kuwa sehemu ya kikosi cha Azam FC kinachoshiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi 2021, lakini madaktari wake wamemruhusu kuanza mazoezi kuanzia Januari 17, ambapo ni wazi michuano ya Mapinduzi itakuwa imeisha hivyo anaweza kusafiri na kikosi kama sehemu ya kwenda kujifunza tu na siyo kucheza.” Amesema Thabit.
Kikosi cha Azam FC jana usiku kilicheza mchezo wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mlandege FC, na kuambuliamatokeo ya 1-1, huku mshambuliaji mpya wa klabu hiyo kutoka DR Congo Mpiana Monzinzi akifunga bao lake la kwanza tangu alipowasili nchini mwezi uliopita.