Klabu ya Asenal bado ina nia ya kumsajili Dugtas Luiz wa Aston Villa, baada ya ofa zao kadhaa walizopeleka kukataliwa.

Arsenal wamesalia na nia ya kutaka kumsajili Douglas Luiz kutoka Aston Villa kufuatia mwanzo wake mzuri wa msimu wa 2023/24.

Vyanzo vimethilbitisha kuwa, The Gunners wanataka kuongeza kiungo mwingine kwenye safu yao wakati wa dirisha la usajili la Januari 2024, na wanatafuta nyota kutoka Ulaya na Amerika Kusini.

Arsenal kwa muda mrefu imekuwa ikivutiwa na Luiz, ambaye amekuwa bora sana kwa sasa hususan msimu huu 2023/24.

Mwishoni mwa juma lililopita alifunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 dhidi ya West Ham United, akiendeleza msururu wake wa kufunga katika mechi za nyumbani za Premier zikifikia mechi sita mfululizo.

Hapo awali Arsenal ilijaribu kutupa ndoano kwa Luiz majira ya joto mwaka 2022, na kutoa ofa tatu, bei ya juu zaidi ya Pauni 25m lakini ikapigwa chini.

Bosi wa The Gunners, Mikel Arteta na Mkurugenzi wa Michezo, Edu Gaspar wote wanamkubali sana Luiz. Arteta anamfahamu kiungo huyo tangu enzi zake akiwa kocha msaidizi wa Manchester City, ambapo aliitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili.

Fedha za Kigeni: Wafanyabiashara msitumie madalali - BoT
Ricardo Ferreira atamba kuibanjua Young Africans