Bondia Abdalah Pazi, maarufu kama ‘Dullah Mbabe’ leo amerejea nchini na kupokelewa na umati wa mashabiki ambao walijitokeza uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kumpokea baada ya kuibuka na ubingwa WBO nchini China na kuweza kuitangaza vyema Tanzania kwa upande wa michezo.

Mbabe amerejea baada ya kumtwanga mpinzani wake kwa ‘TKO’ raia wa China, Zulipikaer Maimaitiali katika raundi ya tatu na kubeba ubingwa wa Super Middle wa WBO Asian Pacific.

Baada ya kurejea nchini Mbabe amesema kuwa ni furaha  kwake kupeperusha bendera ya Taifa na kurejea na ubingwa.

“Kwangu ni furaha kubwa kubeba ubingwa na kurejea nao katika ardhi ya Tanzania, shukrani kwa mashabiki kwa sapoti yao kubwa,” amesema Dullah Mbabe.

Mbali na Dullah Mbabe hivi karibuni bondia mwengine aliyeitamba ughaibuni kwa kupata ushindi nchini Serbia ni Bruno Tarimo maarufu  kama Vifua viwili ambaye ameshinda ubingwa wa IBF.

Bondia vifua viwili alimshinda Serif Gurdijeljec katika pambano ambalo limefanyika usiku wa kuamkia siku ya jumapili septemba mosi na kuweza kuifanya Tanzania kupata ushindi wa pili mfululizo upande wa masumbwi baada ya bondia Dullah Mbabe.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 3, 2019
Mrithi wa Tundu Lissu kuapishwa kesho bungeni