Bondia Dullah Mbabe na mpinzani wake Amour Shehe Haji wameshiriki katika utambulisho wa pambano lao la fainali wa champion wa kitaa litakalo fanyika Februari 20, 2022 katika Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.

Wakizungumza baada ya utambulisho huo uliofanyika katika viwanja vya Las Vegas Mabibo jijini Dar es salaam, Mbabe na Haji wamewataka mashabiki wa mchezo wa ngumi kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kushuhudia pambano lao na mapambano mengine huku kila mmoja akitamba kumtwanga mwenzake.

“Nilikua na matatizo ya kiafya na sasa naimarika kwa hiyo siku hiyo nitajaribu makombola yangu kama yako vizuri,” amesema Mbabe.

“Huu ni wakati wa mabadiliko na nikisema wakati wa mabadiliko naomba mnielewe na mimi sio begi la mazoezi kwahiyo Dullah Mbabe ajiandae,” amesema Haji.

Kwa upande wake muandaaji wa pambano hilo, Selemani Semunyu amewaomba wadau wa nguvu kujitokeza kwa wingi kwe fainali hiyo yenye mapambano zaidi ya 15 yatakayojumuisha mabondia mbalimbali wa hapa nchini.

Luis Miquissone hajaikatia tamaa Simba SC
Shaffih Dauda amvaa Rais TFF