Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ anatarajia kupanda ulingoni kwa mara ya pili kurudiana na kiboko yake, Tshimanga Katompa wa DR Congo katika pambano la raundi kumi linalotarajia kupigwa Novemba 25, mwaka huu kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

Dullah Mbabe atapanda ulingoni katika pambano hilo la raundi kumi akiwa na rekodi za kuchezea kichapo kizito katika pambano la kwanza ambalo lilipoteza utawala wake nchini.

Pambano hilo ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Red in Lady Promotion chini ya Mbunge wa Viti Maalum, Susan Mwakagenda huku likiwepa jina la The Jungle Fight.

Mbali ya pambano kuu, mabondia wengine watakaopanda ulingoni kwenye pambano hilo Paul Kamata atakayepanda ulingoni dhidi ya Jacob Maganga wakati Loren Japheth akitarajia kuzichapa na Rilwal Liwan wa Nigeria.

Wengine ni Shaban Kaoneka akipewa Kassim Somboko wakati Shaban Ndaro akipewa Saleh Mkalekwa lakini Chiku Idd akitarajia kukiwasha na Leila Macho.

Mkongwe wa Kilimanjaro, Alibaba Tarimo anatarajia kumvaa Karage Suba Mzee wa Gadi Kibanda huku Sarah Alex “Miss GB wa Chuga akitarajia kumalizana na Tatiana Ezekiel.

Gamondi afichua mazito Young Africans
Rais Samia atoa ndege Taifa Stars