Mwanamuziki wa muda mrefu kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva Dully Sykes ameweka wazi kuwa yeye ni miongoni mwa wakongwe wa muziki huo mwenye mchango mkubwa.
Dully Sykes ameyasema hayo kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Planet Bongo ambapo alihitaji kudhihirisha kuwa mchango wake haujaishia kwenye kufungua milango ya muziki wa kuimba Tanzania bali hata katika kuvishika na kuvinyanyua vipaji vya wasanii wachanga.
Dully amesema kuwa wamefanikiwa kulea vipaji vya wasanii wengi ambao kwa sasa ni wakubwa na wanaofanya vizuri kwenye kiwanda cha muziki nchini na hata nje ya mipaka akimtaja mwanamuzuki Darassa kuwa mmoja wa wasanii waliopitia kwenye mikono yake kabla ya kuwa nyota mkubwa wa muziki wa bongo fleva hivi sasa.
“Mimi huwa ni muongeaji lakini sio mtu ambaye huwa nataka credit zangu, hivi ulikuwa unajua kama Darassa amepita Misifas Camp? Sipendi kujipakulia minyama kwasababu kiukweli katika wakongwe ambao wametunza wasanii ambao leo wanafanya vizuri, Mimi Sijawahi Kujizungumzia,” alisema.
“Kama Nikitaka Kujizungumzia, kina Darassa wote wamepitia mikononi mwangu na ni wakubwa, sasa hivi ni wa kimataifa, hawa na wasanii wengine sitaki kuwataja hapa wote, huwa sina desturi ya kuzungumzia hivyo vitu,” aliongeza.
Na havina faida, Kama umeumbwa uwanaume na una akili huwezi ukazungumza kwamba flani flani nimewasaidia, haipendezi utasubiri wenyewe watasema.” Aliongeza Dully