Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Dunia kwa sasa inakabiliwa na changamoto za harakati kuhusu kupenyeza uharibifu wa maadili hivyo kupitia utaratibu wa mashindano ya kuhifadhi Qur’aan ni jitihada za kuimarisha maadili mema kwa kuwalea vijana kiroho na kitabia.

Ameyasema hayo katika fainali za Tuzo za Kimataifa za Qur’aan zilizoandaliwa na Jumuiya ya kuhifadhi Quran Tanzania ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amewahimiza Vijana waumini wa dini ya Kiislamu kuisoma Quran na kushikamana kupitia mafunzo yake kwa kuleta tija kwa jamii na kuendelea kuyalinda maadili mema Kizazi cha sasa na kijacho.

Mashindano hayo ya Tuzo za kimataifa za Quran Mwaka 2023 yametimiza miaka 31 tangu kuanzishwa kwake yameshirikisha nchi zaidi ya kumi na tisa kutoka mabara tofauti na washiriki maalumu wa Adhana kutoka nchi tatu.

Kocha Simba SC ashikilia hatma ya Dilunga
Tukio la Hakimi amemkopi 'mwamba' Gabriel Villa