Taarifa zinaeleza kuwa, Klabu ya Paris Saint-Germain imekubaliana na nyota wa Juventus, Dusan Vlahovic, huku ikielezwa huenda akasaini mkataba wa miaka mitano.
Imeelezwa kuwa, Paris Saint-Germain, wapo kwenye mpango wa kukamilisha dili ya Vlahovic kabla ya dirisha la usajili huu wa majira ya joto halijafungwa.
Ripoti zinaeleza kuwa, Vlahovic atapewa mkataba wa miaka mitano na mshahara kiasi cha euro 11m kwa mwaka pamoja na bonasi.
Katika kukamilisha dili hilo, Paris Saint-Germain wameambiwa na Juventus watoe ada ya euro 80m kuchumua straika huyo.
Paris Saint-Germain wanafanya uamuzi wa kumnunua Vlahovic wakiwa na mpango wa kumuuza Neymar, huku wakihakikisha Kylian Mbappe anasalia kikosini hapo.
Juventus walimsajili Vlahovic kutoka Fiorentina akiwa ni mbadala ya Cristiano Ronaldo ambaye aliondoka Juventus 2021.
Inaelezwa kuwa, mpango wa Vlahovic kutua kikosini ni mpango wa kocha mpya wa timu hiyo, Luis Enrique.