Mshambuliaji wa Argentina na mabingwa wa Italia Juventus FC Paulo Bruno Exequiel Dybala, ametajwa kuwa mshindi wa tuzo ya heshima ya MVP kwa msimu 2019-20, baada ya kucheza kwa kiwango kizuri na kuisadia klabu yake kutetea ubingwa wa Serie A.

Dybala ametajwa kama mshindi wa tuzo hiyo ya heshima (MVP), huku akimbwaga mshambuliaji mwenzake wa Juventus FC Cristiano Ronaldo, ambaye alidhaniniwa huenda angekua mshindi.

Dybala amefunga mabao 11 na kutoa pasi za mabao sita katika ligi ya Sirie A, huku The Bianconeri wakifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi ya Italia kwa ya mara tisa mfululizo.

Mshambuliaji huyo aliongoza kwenye viwango, hii ni kwa mujibu wa uchunguzi wa Stats Performs, ambapo waliweza kukusanya takwimu kutoka kwenye michuano ya Coppa Italia na Supercoppa Italiana pamoja na Serie A.

Ronaldo ameifungia Juve mabao 31 lakini Mreno huyo aliangushwa na mshambuliaji bora wa msimu Ciro Immobile, ambaye alifikia rekodi ya kufunga magoli mengi kwa msimu mmoja rekodi ya mkongwe Gonzalo Higuan kwa kufunga mabao 36 ndani ya msimu huu akiwa na klabu ya SS Lazio.

Kulikuwa na mafaniko ya juu kabisa kwa mabingwa, walakini Wojciech Szcesny alitajwa kama Golikipa bora, na beki wa Inter Stefan de Vrij alitajwa kama beki bora.

Alejandro Gomez aliyeisaidia Atalanta kumaliza katika nafasi ya tatu alipata tuzo ya kiungo bora wa msimu, Dejan Kulusevski alitajwa kama mchezaji chipukizi wa msimu baada ya kuwa na msimu wa kuvutia akitokea Parma kwa mkopo.

” Ulikuwa ni mwaka mgumu, lakini hawa wachezaji wametuonesha vipaji vyao katika michezo yote waliyo cheza na walicheza kwa kiwango kikubwa,” Luigi De Siervo Mkurugenzi mkuu wa Serie A alisema alipokuwa akiwatangaza washindi wa tuzo hizo.

Magufuli kuchukua Fomu wiki hii
Polepole''CHADEMA waombe radhi kubadili wimbo wa Taifa''