Uongozi wa klabu ya Simba SC umevunja mkataba na aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi cha ‘wana Msimbazi’ Dylan Kerr kwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili na kufikia uamuzi huo.

Makamu Mwenyekiti wa Simba SC Geofrey Ntyange ‘Kaburu’ amesema pande zote mbili (Simba SC na kocha Dylan Kerr) wamekubaliana kuvunja mkataba baada ya kukaa na kujadiliana kwa kirefu.

“Tumevunja mkataba na Kerr kwa makubaliano ya pande mbili baada ya kukaa na kujadiliana hatimaye tukafikia uamuzi huo”, amesema Kaburu ambaye alikuwepo Zanzibar akishuhudia mchezo kati ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar ambao Simba ilitupwa nje ya mashindano ya Mapinduzi katika hatua ya nusu fainali.

Katika hatua nyingine, kocha mpya wa klabu hiyo Jackson Mayanja ambaye amesaini mkataba na klabu hiyo siku chache zilizopita kama kocha msaidizi atachukua mikoba ya Kerr kwa muda wote ambao Simba itakuwa ikifanya mchakato wa kumpata mrithi wa Kerr.

Serikali Yakata Rufaa Kupinga kuachiwa huru kwa Sheikh Ponda
Atletico Madrid Yakataa Ofa Ya Usajili Wa Saul Niguez