Kocha wa Simba, wakati huo huo
Katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC, Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kushangilia kwa staili ya kupiga simu, wakitumia viatu.
Simba itaivaa Jamhuri katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Mapinduzi, Kerr raia wa Uingereza amesema wamejiandaa, wako tayari.
“Tunajua tutaanza na ugumu kwa kuwa ukubwa wa Simba unafanya kila timu unayocheza nayo ijiandae na kupania lakini tumejiandaa na tunaamini kabisa tupo tayari, tunataka kushinda,” aliseka Kerr.
Watani wao Yanga tayari wameanza michuano hiyo kwa kishindo kwa kuipachika Mafunzo kwa mabao 3-0 katika mechi yake ya kwanza ya michuano hiyo ambayo Simba ndiyo bingwa mtetezi.
Wakati huo huo kikosi cha JKU cha kisiwani Unguja (Zanzibar) kimeanza vibaya michuano hiyo kwa kufungwa mabao matatu kwa moja dhidi ya timu ya mamlaka ya mapato nchini Uganda URA.

G - Love aeleza jinsi Mr. Blue, Ebby Skillz walivyomkera
Pellegrini Aendelea Kujitisha Kwa Kivuli Chake Man City