Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya Simba, Dylan Kerr amesema bado yupo jijini Dar es salaam akisubiri malipo yake ikiwemo mshahara wa miezi miwili iliyopita.

Akizungumza kwa njia ya simu, Kerr alisema hangependa kuzungumzia sana masuala yake na klabu hiyo kupitia vyombo vya habari.

“Sitaki kuzungumzia sana suala la kufukuzwa kwangu lakini kwa kifupi bado nipo nasubiri viongozi wangu waniite ili tumalize suala hili,”alisema.

Alisema bado anafuatilia malipo yake ikiwemo mishahara ya miezi miwili ambayo uongozi wa Simba ulikuwa haukumlipa.

“Bado nafuatilia malipo yangu, sijalipwa miezi miwili kwa hiyo naomba uniache.Sipendi kuongea sana,” alisisitiza

Hii ina maana kwamba Muingereza huyo alifanya kazi ya kujitolea katika miezi ya Novemba na Disemba mwaka jana, jambo ambalo huenda likawa limesababisha timu kucheza bila ya morali.

Kerr ameiongoza Simba katika mechi 13 za Ligi Kuu Bara na nane kati ya hizo alishinda, sare tatu na alipoteza mbili.

Kwa upande wa mechi za jumla tangu atue nchini kuinoa timu hiyo, Kerr ameiongoza Simba jumla ya mechi 30 ambapo 19 kati ya hizo alishindsa na kufungwa mechi 5 huku 6 ikiwa ni sare.

Mexime: Mtibwa Sugar Hatuna Bahati Na Kombe La Mapinduzi
Namelock Sokoine akabidhiwa mkoba wa Lowassa Monduli