Msanii wa maigizo ya vichekesho, Anastasia Exavery maarufu kama Ebitoke ambaye amekuwa akifanya kazi Timamu TV ametangaza kuondoka kuifanyia kazi TV hiyo mara baada ya mkataba wake kumalizika.

Ebitoke amesema hayo kupitia ukurasa wake wa instagram na kudai kuwa kwa sasa atakuwa anafanya kazi na TV nyingine.

”Napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu mashabiki na watu wote wanaonitazama na kusoma ujumbe huu, Kuanzia sasa nitakuwa nikifanya kazi zangu nje ya Timamu TV nikimaanisha mkataba wangu na Timamu TV umeisha” ameandika Ebitoke.

Aidha ametoa shukrani zake za dhati kwa uongozi mzima wa Timamu TV kwa kushirikiana pamoja katika kuhakikisha wanafanya kazi nzuri, lakini pia amewashukuru wafanyakazi wenzake ambao amekuwa akishirikiana nao katika kutengeneza maigizo mafupi ya vichekesho ambao ni @ Bwanamjeshi na @Mr. Beneficial.

Mbali na hatua hiyo  Ebitoke ameenda mbali zaidi kwa kufuta video zake zote za kazi alizofanya akiwa chini ya uongozi wa Timamu TV kwenye ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi Milioni 1.

Aidha hajasema baada ya kumaliza mkataba wake na Timamu TV atasajiliwa na TV gani nyingine kuendeleza fani yake ya uchekeshaji.

Rais Magufuli akazia sababu za kutosafiri nje...
Mkhitaryan kuikosa Qarabag, ahofia usalama wake