Klabu ya AFC Bournemouth inaangalia uwezekano wa kuwasilisha ofa ya usajili wa beki na nahodha wa Chelsea John Terry, katika kipindi hiki cha majira ya baridi (Dirisha Dogo).
Taarifa zinameeleza kuwa, meneja wa AFC Bournemouth Eddie Howe ana mipango ya kumtumia Terry kwa mokopo, kwa kuamini uzoefu wake utaisaidia safu yake ya ulinzi kuelekea mwishoni mwa msimu huu.
Hata hivyo kigezo cha ushindani wa nafasi katika safu ya ulinzi ya Chelsea, nacho kinatumiwa na Eddie Howe kama sehemu ya kuamini huenda akampata Terry kwa urahisi kabla ya dirisha halijafungwa mwishoni mwa mwezi huu.
Safu ya Chelsea kwa sasa ina watu kama Gary Cahill, David Luiz Cesar Azpilicueta pamoja na Kurt Zouma ambaye yu njiani kurejea katika hali yake kiafya, baada ya kuuguza majeraha ya goti kwa muda mrefu.
Terry pia ana nafasi finyu ya kusaini mkataba mpya ambao utamuwezesha kuendelea kuitumikia Chelsea, kufuatia mkataba wake kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.