Siku moja baada ya kuhusishwa na taarifa za kupewa kipaumbele cha kumrithi meneja wa Arsenal Arsene Wenger huko kaskazini mwa jijini London, meneja wa Bournemouth Eddie Howe amezipa kisogo tetesi hizo.

Howe ameonyesha hali hiyo, alipokua katika mkutano na waandishi wa habari ambao ulizungumza mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo kikosi chake kitapambana na West Bromwich Albion katika mshike mshike wa ligi ya nchini England (PL).

Howe aliulizwa swali na waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wake hii leo huko Dean Court, lakini alijibu kwa kusema hana mpango huo zaidi ya kuangalia ajira yake kwa sasa.

“Sio wakati wa kuamini taarifa za kuhusishwa na ajira ya Arsenal, natambua jukumu lililopo mbele yangu la kuhakikisha Bournemouth inafanya vyema katika ligi pamoja na michuano mingine tunayoshiriki.

“Ninapendezwa na mazingira ya hapa na ninaamini uwepo wangu hapa una heshima kubwa sana, tofauti na mahala pengine ambapo jina langu limeanza kutajwa.” Amesema Howe

Katika hatua nyingine Howe amesisistiza kuheshimu mawazo ya kila mmoja ambaye ataingia katika ulingo wa kumpa nafasi ya kupata ajira ya kuwa meneja wa Arsenal, lakini akasema bado msimamo wake wa kuendelea kufanya kazi ya kumtumikia muajiri wake wa sasa itaendelea kama kawaida.

Yaya Toure Afikiria Kuongeza Mkataba Man City
Huruma Ya FIFA Yaibeba Sunderland, Wafanya Usajili Nje Ya Muda