Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Eden Hazard amempiga dongo kiaina aliyekua meneja wa Chelsea Jose Mourinho ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Man Utd, kwa kumsifia Antonio Conte aliyekabidhiwa jahazi la The Blues.

Hazard alionekana kuwa na wakati mgumu wa kucheza vyema katika nafasi yake uwanjani wakati wa utawala wa Mourinho, jambo ambalo liliibua hisia kwa mashabiki wengi wa soka duniani huenda wawili hao walikua na ugomvi wa nje ya uwanja.

Hazard amesema amekua na maono tofauti ya kikosi cha Chelsea tangu kilipoanza kuwa chini ya meneja mpya kutoka nchini Italia Antonio Conte, na hadhani kama utawala huo uliwahi kutokea tangu aliposajiliwa mwaka 2012 akitokea Lille ya nchini Ufaransa.

“Conte anamuamini kila mmoja wetu kikosini, na hana tabia za kuwa na hasira dhidi ya wachezaji zaidi ya kutoa maelekezo pale linapotokea jambo tofauti na matarajio yake,”

“Kila mmoja wetu amekua akicheza kwa kujielewa na kwa nafasi yake uwanjani, jambo ambalo limedhihirisha Conte anajua anachokifanya.” amesema Hazard alipohojiwa na gazeti la  L’Equipe Ufaransa.

Uhasama Wa Wenger Na Mourinho Wadhihiri, Waibua Kituko UEFA
Ray Parlour Ampendekeza Diego Simeone Arsenal