Mlinda mlango wa Man City Ederson ameibukia katika mazoezi ya kikosi cha klabu hiyo, baada ya kupata majeraha ya uso, mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England dhidi ya Liverpool.

Ederson ameibukia mazoezini, akiwa katika muonekano tofauti na alivyozoeleka, kutokana na kuzuia kichwa (skullcap) alichokua amekivaa, kutokana na kadhia aliyoipata mwishoni mwa juma lililopita.

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane, alimpiga tele la uso mlinda mlango huyo kutoka nchini Brazil na kumsababishia maumivu makali, ambayo yalimzuia kuendelea na mchezo.

Ederson alilazimika kupatiwa huduma ya kwanza kwa muda wa dakika nane uwanjani, kabla ya kutolewa uwanjani kwa uangalizi mkubwa wa kitabibu.

Mashabiki wengi wa soka duniani waliofuatilia mchezo huo ambao ulimalizika kwa Liverpool kufungwa mabao matano kwa sifuri, waliamini huenda mlinda mlango huyo angeendelea kukaa nje kwa siku kadhaa, lakini kuonekana kwake katika mazoezi kumewashtua.

Ederson aliweka picha za jeraha lake la uso katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, ambayo ilionyesha namna alivyoshonwa nyuzi kadhaa kutokana na ukubwa wa sehemu iliyokua imepasuka.

Ederson's face looked more than sore after the Sadio Mane collision

Hata hivyo bado haijafahamika kama Ederson atakuwa sehemu ya kikosi cha Man city ambacho kitacheza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Feyenoord hapo kesho.

Watumishi wa umma waonywa kuhusu taarifa za Serikali
Kozi za ukocha ngazi ya awali na kati mikoani