Mchambuzi wa Michezo nchini Tanzania Edo Kumwembe amesema kuna ulazima Michezo ya Soka la Afrika ikachezwa bila usaidizi wa Teknolojia ya kumsaidia Mwamuzi (VAR), kufuatia maamuzi yake kupuuzwa na kutofanyiwa kazi.

Edo Kumwembe ambaye pia ni Mwandishi wa Habari za Michezo nchini Tanzania ametoa kauli hiyo, kufuatia tukio la mchezo wa jana Jumapili (April 24) ambapo Mfungaji wa bao la Orlando Pirates Kwame Peprah kudaiwa alikua ameotea kabla ya kufunga bao dhidi ya Simba SC Uwanja wa Orlando Afrika Kusini.

Edo amesema Teknologia ya VAR imeshindwa kuheshimiwa katika soka la Bara la Afrika na hadhani kama ina umuhimu kwa sasa, kwa sababu inaendelea kuwaumbua waamuzi wengi wanaoshindwa kuitumia kama msaidizi.
“VAR imekuaja kutuumbua zaidi ‘Afrika’ ni bora ingeondolewa kabisa katika mashindano.”

“Inasikitisha kuona maamuzi ya VAR yanapuuzwa na hayafuatwi kama ilivyotarajiwa na mashabiki wa soka letu hapa Afrika, sasa kuna umuhimu gani wa Teknolojia hii kuendelea kutumika.”

“Ukiangalia wanaoiendesha hii VAR ni watu kama sisi, kwa hiyo wanaweza kuamua kuuchuna na wakafanya mambo yao kama ulivyoona katika mchezo wa jana, kwa hakika halikua bao halali kwa Orlando japo mwamuzi alisubiri kwa zaidi ya dakika moja, picha ikaja ikamuumbua na kila mmoja ameona mfungaji alikua amezidi.” amesema Edo Kumwembe

Simba SC iliondoshwa kwenye Michuano ya Kombe la SHirikisho Barani Afrika jana Jumapili (April 24), kwa changamoto ya mikwaju wa Penati 4-3 dhidi ya Orlando Pirates iliyokua nyumbani Orlando Stadium Afrika Kusini, baada ya kufunga bao 1-0 ndani ya dakika 90 na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya sare ya 1-1, na hii ni baada ya Mnyama kushinda 1-0 nyumbani Uwanja wa Mkapa Jumapili (April 17).

Nasreddine Nabi: Wachezaji wote wapo salama
Ahmed Ally: Simba SC hatujapiga hatua kwenda nyuma