Kauli nyingine hutolewa kwa utani lakini ukizifuatilia na kuzifanyia kazi, unaweza kuwa tofauti dhidi ya wengine kimaendeleo.

Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa Michezo Edo Kumwembe, ametuma ujumbe Young Africans kama utani lakini ukiuchukua na kuufanyia kazi japo kwa dakika tano, utagundua mdau huyu anaitakia mema klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Kumwembe ameutaka Uongozi wa Young Africans kutoa japo shilingi Bilion 3, ili kukamilisha mradi wa uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo (WANANCHI COMPLEX) utakaojengwa Kigamboni Dar es salaam.

Shilingi Bilion 3 alizotaka zitumike kwenye mradi wa uwanja (Wananchi Complex), zitatokana na mkataba mnono wa Young Africans waliosaini hii leo na kampuni ya Azam Media jijini Dar es salaam.

Ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook:
“Yanga hizo bilioni 34…basi wekenii bilioni 3 tu mfanye hivi muwe timu kubwa na kongwe kwa pamoja…sometimes kuna tofauti kati ya timu kubwa na kongwe…”

Mapema hii leo Alhamis (Julai 08), Uongozi wa Kampuni ya Azam Media ulisaini mkataba wa miaka 10 na klabu ya Young Africans wa uchakataji maudhui (Media Partnership), wenye thamani ya Shilingi bilioni 34.8.

Mkataba huu unaifanya Azam TV kurusha matukio yote ya Young Africans kama michezo ya kirafiki, Mazoezi, Exclusive Interview za Viongozi na Wachezaji na matukio yote yanayoihusu klabu hiyo.

Ndoto za ubingwa Young Africans bado zipo
Ramos akamilisha PSG