Majogoo wa jiji (Liverpopol) wametupwa nje ya michuano ya kombe la ligi nchini England (EFL CUP), baada ya kukubali kisago cha bao moja kwa sifuri dhidi ya Southampton.
Liverpool ambao walipewa nafasi kubwa ya kutinga katika fainali ya michuano hiyo, walikubali kupoteza mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo, kutokana na umakini mkubwa ulioonyeshwa na kikosi cha Southampton.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali, Liverpool walikubali kufungwa bao moja kwa sifuri, na hivyo wametupwa nje kwa jumla ya mabao mawili kwa sifuri.
Bao pekee na la ushindi kwa Southampton lilifungwa na Shane Long katika daikika ya 90.
Hii inakua ni mara ya kwanza kwa Southampton kutinga katika hatua ya fainali ya michuano ya kombe la ligi (EFL CUP), baada ya miaka 38.
Hii leo mchezo wa pili wa nusu fainali utachezwa katika uwanja wa KCOM ambapo wenyeji Hull City watakua na shughuli ya kuwakabili Man Utd.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza Man Utd walichomoza ushindi wa mabao mawili kwa moja, yaliyofungwa na Juan Mata na Marouane Fellaini.