Halmashauri ya Jiji la Mbeya, imetakiwa kuongeza jitihada ya kuwawezesha Wanafunzi wa kike, ili waweze kupata elimu katika mazingira rafiki hasa wakati wa siku zao za hedhi.

Hayo, yamebainishwa hii leo Agosti 15, 2023 na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson wakati wa hafla ya kukabidhi taulo za kike 4000 kupitia mfuko wa Halmashauri kwa Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi za Serikali, iliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya wasichana Loleza.

Amesema, bado idadi ya hitaji hilo inayotolewa ni ndogo kulingana na uhitaji wake na ameahidi kushirikiana nao ili kuhakikisha taulo nyingi zaidi zinazopatikana ili kukidhi mahitaji.

Awali, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Dormohamed Issa, alimshukuru na kumpongeza Dkt. Tulia kwa jitihada anazozizifanya katika Jiji hilo, ikiwemo kuwaunganisha Wananchi na Serikali yao.

Polisi Jamii Cup DPA kuchangia benki Damu Salama
Benjamin Pavard aibadilikia Bayern Munich