Wadau wa Elimu wametakiwa kuungana na serikali kutoa misaada katika kuboresha miundombinu ya shule za msingi na Sekondari kutokana na matarajio ya Ongezeko kubwa la udahili wa wanafunzi wa sekondari ya juu mwaka 2022.

Akiongea katika ufunguzi wa Kikao cha Asasi zinazotoa huduma katika elimu msingi Mgeni Rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde, amesema Serikali inatarajia kuwa na ongezeko kubwa la udahili wa wanafunzi mwaka 2022 kutokana na sera ya elimu bure ambayo ilianzishwa na serikali ya awamu ya tano.

Aidha Serikali awamu ya sita imeendelea kutoa elimu msingi bila malipo ambapo uandikishaji wa Watoto wa elimu ya awali umeongezeka kutoka 86.1% mwaka 2020 hadi 94% mwaka 2021.

Naibu Waziri wa TAMISEMI Silinde amesema matarajio ya serikali katika kikao kazi hicho ni kujadiliana na kuhakikisha zinapatikana mbinu bora Zaidi katika kuimarisha elimu msingi na Sekondari nchini.

Sambamba na hayo yote Naibu Waziri Silinde ametoa rai kwa Asasi zote za elimu nchini kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia vipaumbele vya serikali na vifuate na kuhesmu sheria kanuni na taratibu za nchi, hivyo katika mambo mtakayokubaliana asasi zote zijikite kutekeleza miradi ambayo serikali inatarajia”

Naye Katibu mkuu Elimu Pr Riziki shemdoe amesema wadau wa elimu ni muhimu kwa serikali kwa sababu nguvu zao katika elimu ni kubwa zikiunganishwa na za serikali maendeleo ya elimu nchini yanakua makubwa.

Kikao cha wadau wa elimu chenye Kauli mbiu “tupange na kutekeleza kwa Pamoja Miradi yenye tija kwa maendeleo ya Elimu Msingi” kinafanyika kwa siku 3 mkoani Dodoma na wadau wa elimu wanawasilisha miradi yao ukiwemo wa Mwalimu Tabuleti wa data Vision International itakayoingizwa katika mipango ya serikali na kutekelezwa hapo baadae mkoani Geita.

Mwandishi Zuhura Makuka

Waziri aagiza Askofu Gwajima akamatwe
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 17, 2021