Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, amewaagiza Tume ya Taifa Sayansi na Teknolojia COSTECH kuwaelimisha wabunifu umuhimu wa kuhakikisha kuwa ubunifu na uvumbuzi wao unatambuliwa na kupewa hatimiliki.

Ameyasema hayo wakati akifunga maonesho ya Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

“Elimu kuhusu hakimiliki ni muhimu kwani itawawezesha wabunifu kulinda ubunifu wao, Wekeni mikakati ya kuwaelimisha wabunifu wachanga husasan walioko katika sekta isiyo rasmi kuhusu umuhimu wa kuwa na hakimiliki,”. amesema Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa anaitaji kuona mabadilliko ya haraka kwenye suala la hatimiliki za wabunifu ili kukuza idadi ya maombi ya hatimilki za wabunifu kutoka Tanzania kwani hadi sasa idadi ya maombi yaliyowasilishwa kutoka Tanzania ni ndogo sana ikilinganishwa na maombi kutoka nchi jirani.

“Takwimu zilizotolewa na Shirika la Hatimiliki Duniani (World Intellectual Property Organization – WIPO) zinazoonesha kwa mwaka 2020, Tanzania iliwasilisha maombi ya hatimiliki nane tu, ikilinganishwa na nchi moja ya jirani iliyowasilisha maombi ya hatimiliki 372; na Afrika Kusini iliyowasilisha maombi ya hatimiliki 1,514,”. Amesema Majaliwa.

Aidha Kassimu majaliwa amewapongeza wabunifu wote walioshiriki mashindano hayo ya MAAKISATU yalifanyika jijini Dodoma.

Hawa ndio wasanii wenye mkwanja mrefu zaidi Afrika 2021
Miradi ya maji kukamilika ifikapo 2025