“Nikiipa mgongo CORONA, 2020 umekuwa ni mwaka wa kuijenga timu ya WANANCHI, YOUNG AFRICANS SC @yangasc

Usajili wa wachezaji bora, benchi la ufundi imara na uongozi bora zimekuwa nguzo katika maendeleo ya klabu yetu.

TRANSFORMATION PROJECT ndio tegemeo letu katika uimara wa kudumu wa timu yetu. Muundo wa mfumo wa uongozi (MANAGEMENT STRUCTURE ) na Mfumo wa kuwajumuisha wanachama ( FAN ENGAGEMENT ) katika kuongeza thamani ya timu yetu umeandaliwa na kusimamiwa kwa uweledi mkubwa kwa ushauri wa @laliga huku tukifungua mahusiano ya ushirikiano na klabu ya @sevillafc

Kujitoa kwetu kuleta matokeo chanya kwa kuiweka timu yetu katika mazingira bora ya kiushindani huku tuking’ara kwa jezi bora zenue mvuto, kambi bora na kisasa, vifaa bora vya mazoezi na usimamizi wenye weledi na mapenzi makubwa umepelekea leo hii kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi ya VODACOM 2020/21 tukiwa kileleni bila ya kupoteza mchezo wowote! Kongole kwa ujumla wetu, haya sasa ndio MATOKEO CHANYA.

Kuelekea 2021, tumuombe mola atupe kheri na baraka. Ukawe ni mwaka yenye neema kwetu, kwa TAIFA LETU na ULIMWENGU kwa ujumla wake.

DAIMA MBELE NYUMA MWIKO. “

Mpango lishe 2021 kunusuru utapiamlo Tanzania
Disko toto, Uchomaji matairi marufuku mwakampya

Comments

comments