Soka litarejea England katika michuano ya Euro itakayofanyika mwaka 2028 baada ya Uturuki kujiondoa rasmi kwenye mbio za kuwania uenyeji.

Zabuni inayoongozwa na chama cha soka England ‘FA’ inayojumuisha mataifa matano shirikishi ya Uingereza (Wales, Ireland Kaskazini, Scotland na England) ina hakika kutangazwa kuwa wenyeji wa michuano hiyo Jumanne (Oktoba 10) kutokana na uthibitisho wa UEFA kwamba imeridhia Uturuki kujitoa.

Hilo linaacha nafasi kwa Uingereza kuwa mgombea pekee, huku chaguo la mwenyeji kuamuliwa rasmi katika mkutano wa Kamati Kuu ya UEFA Jumatatu (Oktoba 09) na kisha kuthibitishwa hadharani siku inayofuata.

Gazeti la Sun Sport liliripoti Julai mwaka huu kwamba Uturuki ilitambua Uingereza itashinda baada ya kujitosa katika kinyang’anyiro cha maombi ya kuwania kuwa mwenyeji wa Fainali za Ulaya za 2028.

Imeelezwa Uturuki imejipanga kuandaa michuano ya Euro ya mwaka 2032 ikishirishiaka na Italia.

UEFA ilitoa taarifa baada ya Uturuki kujiondoa: “Katika taarifa iliyotolewa Julai 28 mwaka huu, Italia na Uturuki zilituma maombi ya kuandaa michuano ya Euro itakayofanyika mwaka 2032.

Mchakato huo utafanyiwa kazi na kamati ya UEFA kabla ya kutoa majibu rasmi. Kwa hiyo maombi ya Uturuki ya kuandaa EURO 2028 sasa yameondolewa.

Washindi wa zabuni za mashindano yote mawili bado wanasubiri kuidhinishwa na Kamati ya Utendaji katika mkutano wake utakaofanyika Nyon-Uswiz Jumanne (Oktoba 10).

Wembley itakuwa moja ya viwanja sita vya Uingereza vitakavyotumika katika michuano hiyo, viwanja ni Villa Park, St James’ Park.

Etihad, uwanja mpya wa Everton huko Bramley Moore Dock na Uwanja wa Tottenham Hotspur.

NGO's zatakiwa kuheshimu, kulinda maadili ya Kitanzania
Polisi feki mikononi mwa Polisi, wapo wa tuhuma za mauaji