Mabingwa wa Nigeria, Enyimba fc wamesitisha mpango wa kuweka kambi jijini Dar kujiandaa na pambano lao la Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa wa Uganda, Vipers.

Mabingwa hao mara mbili wa Afrika walitarajia kucheza mechi ya kujipima nguvu na mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga kabla ya kusafiri kuelekea Uganda.

Msemaji wa Enyimba, Fareil Allaputa ameiambia Soka360 kuwa wamesitisha mpango huo kutokana na muda kuwabana.

” Tulikuwa na mpango wa kuja Dar lakini kwa bahati mbaya sasa haitawezekana kutokana na kubanwa na muda”

Yanga ilitarajia kuutumia mchezo kujiandaa na pambano lao la hatua ya awali ya ligi ya Mabingwa dhidi ya klabu ya Mauritius Cercle de Joachim katikati ya mwezi ujao.

Stephan El Shaarawy Aihama AC Milan
Azam FC Walazimisha Sare Mjini Ndola, Zambia