Ligi Kuu ya England (EPL) imefikia makubaliano ya kusaini mkataba wa haki za matangazo ya televisheni na kampuni za Skynews na TNT wenye thamani ya Pauni Bilioni 6.7 kuonesha mpaka mechi 270 kwa msimu.
Mkataba huo unajumuisha kampuni ya BBC kuendelea kuonesha vipande kwenye siku mechi zinazochezwa.
Mamlaka ya Ligi Kuu ya England ilisema mkataba huo ni wa miaka minne kuanzia msimu wa mwaka 2025-26.
Sky imepewa vifurushi vinne kati ya vitano na wataonesha kiasi kidogo mechi 215 kwa msimu zikiwemo mechi za Jumamosi zitakazoanza saa 11:30 jioni, na siku ya Jumapili saa 8 mchana hadi 10:30 jioni sambamba na mechi za jioni siku ya Jumatatu na Ijumaa.
TNT wa taonesha mechi kiasi kidogo 52 kwà msimu zikiwemo zitakaoanza saa 12:30 Jumamosi na mechi mbili za katikati ya wiki. Sky Sports wataonesha mechi zote za mwisho kwenye kila msimu.
Amazon, ambao wanaonesha mechi 20 kwa msimu kwenye mkataba wa sasa, hawajapata nafasi kwenye makubaliano mapya.
Mkataba wa sasa wa haki za matangazo wenye thamani ya Pauni Bilioni 5 na wa miaka mitatu utafikia kikomo mwishoni mwa msimu wa mwaka 2024-25 na wameruhusiwa kuongeza muda kwa sababu ya madhara ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona.