Tatizo la Saratani limekuwa likiongezeka kila mwaka. Shirika la Afya Duniani linakadiria kuwa kila mwaka wagonjwa wapya wapatao 50,000 hugundulika na Saratani za aina mbalimbali Tanzania.
Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na watoto imetoa njia mbalimbali za kujikinga au kupunguza uwezekano wa kupata saratani. Ambazo ni,
- Epuka kuwa na usito uliokithiri kwa kufanya mazoezi angalau dakika 30 hadi 60 kwa siku, kwa siku tatu au wiki.
- Kula mboga na matunda kwa wingi.
- Epuka vyakula vilivyokobolewa, kwa kula nafaka zisizokobolewa na kutumia aina mbalimbali za mikunde kama maharage, njeger, mbaazi n.k
- Punguza ulaji wa nyama nyekundi yenye mafuta kwa kuoka, au kubanika na kula nyama nyeupe kama za kuku na samaki.
- Epuka mafuta ya wanyama, tumia mafuta ya mimea kama karanga, ufuta na alizeti.
- Epuka unywaji wa pombe uliokithiri, na achana na matumizi ya tumbaku na bidhaa zake.
-
Wajawazito watakiwa kujitokeza kupata huduma za kiafya bure
-
Vitamin D husaidia kupambana na Saratani ya Matiti
Takwimu za mwaka 2016/2017 kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonesha kwamba saratani zinazoongoza nchini ni Saratani ya kizazi 32.8%, saratani ya ngozi 11.7%, saratani ya matiti 12.9%, saratani ya kichwa na shingo 7.6%, saratani ya matezi 5.5%, Saratani ya damu 4.3%, saratani ya kibofu cha mkojo 3.2%, Saratani ya ngozi 2.8%, Saratani ya macho 2.4%.
Katika kuadhimisha siku ya Saratani duniani, inatoa wito kwa watu kupima ugonjwa wa saratani.