Rais wa Uturuki na Waziri Mkuu wa Israel wameendelea kurushiana maneno, huku kila upande ukitumia kauli kali dhidi ya mwengine kutokana na mauaji ya vikosi vya nchi zao kwenye maeneo mengine.
Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki alimuita Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kuwa ni ‘gaidi’ ikiwa ni sehemu ya mashambulizi ya maneno makali baina yao yaliyoanza baada ya yeye Erdogan kuikosoa hatua ya kijeshi ya Israel dhidi ya maandamano katika mpaka wa Gaza.
Aidha, Israel imetetea mauaji ya Wapalestina 15 wakati wa maandamano ya siku ya Ijumaa na Netanyahu alituma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter, akisema jeshi la nchi yake halitafundishwa na watu ambao wanawapiga mabomu raia wasio hatia kwa miaka kadhaa.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, na Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini, wametaka kufanyika kwa uchunguzi huru,