Imefahamika kuwa Kiungo Mshambulaiji kutoka nchini Denmark Christian Eriksen ana nafasi kubwa ya kuendelea kuitumikia klabu ya Brentford, kwa msimu ujao wa 2022-23.

Meneja wa klabu hiyo Thomas Frank amesema bado Eriksen ana nafasi hiyo, kutokana na uwezo wake aliouonyesha tangu alipomsajili, wakati wa Dirisha Dogo la Usajili mwezi Januari.

Uhakika huo wa meneja Thomas Frank, umekuja baada ya klabu za Tottenham, Newcastle na Manchester United kuanza kutajwa katika vita ya kumuwania itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Meneja Thomas Frank amesema: “Siku zote nina matumaini,”

“Siku zote naamini tuna nafasi nzuri sana. Najua ana furaha hapa, anafurahia soka lake. Ni uamuzi ambao utachukuliwa mwishoni mwa msimu.”

Eriksen alianza tena kucheza soka kwa mara nyingine akiwa na klabu ya Brentford inayoshiriki Ligi Kuu ya England baada ya kuzimia alipokuwa akiichezea Denmark kwenye Fainali za Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2020’ mwaka jana, huku akiwekewa kifaa cha pacemaker, baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.

Eriksen amekuwa mchezaji bora wa Brentford na ndiye aliyeshinda katika michezo sita kati ya minane aliyocheza, huku mingine ikitoka sare dhidi ya Tottenham na kisha kupoteza Jumatatu (Mei 02) kwenye Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Manchester United. Eriksen pia alifunga katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Chelsea Aprili 2.

Alipoulizwa jinsi Brentford anajaribu kumshawishi abaki, Frank alisema: “Rahisi sana, ninazungumza naye. Tunawasilisha mipango yetu na kuijadili kwa pamoja.”

Watu wanne wahukumiwa kunyongwa hadi kufa
David Alaba kuikosa Manchester City