Kocha Mkuu wa Man Utd Erik ten Hag amesema ni dhahiri kwa nini klabu hiyo ilimsajili mshambuliaji msimu huu baada ya timu yake kuhangaika mbele ya lango kwenye kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Tottenham Jumamosi (Agosti 19).

United walikuwa wazi juu ya hitaji lao la kuongeza mshambuliaji katika dirisha la uhamisho, huku ESPN ikiripoti hapo awali idara ya usajili ya klabu ilikuwa na hifadhi data ya washambuliaji karibu 1,800 mwanzoni mwa utafutaji wao.

Licha ya Harry Kane kuondoka Spurs msimu huu wa majira ya joto akijiunga na Bayern Munich, United iliamua kumsajili Rasmus Hojlund mwenye umri wa miaka 20, katika mkataba uliojumuisha ada ya Pauni Milioni 64, pamoja na Pauni nyingine Milioni nane katika nyongeza.

Baada ya kuona timu yake ikishindwa kufunga mabao ambayo ni pamoja na kusajili mashuti matatu pekee kati ya 14 yaliyolenga lango kipindi cha kwanza, Ten Hag alisema anaamini kikosi chake kina mabao, lakini alikiri kuwasili kwa Hojlund, ambaye bado hajacheza mechi yake ya kwanza kutokana na kuumia, ni suala la muda.

“Tunaamini wachezaji hawa, wanaweza kufunga mabao. Ni wazi pia kwa nini tulisajili mshambuliaji,” alisema Ten Hag akiwaambia waandishi wa habari.

“Kama yote yataenda vizuri, Marital yuko njiani kurudi, Hojlund pia anakuja, kwa hivyo tutakuwa na wachezaji wengi wa kufunga mabao, Wachezaji uwanjani wanaweza pia kufunga mabao.”

United waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Wolves Jumatatu iliyopita, huku matokeo ya juzi Jumamosi (Agosti 19) yakiongeza mwanzo wao wa polepole wa msimu wa 2023-24 wa Ligi Kuu England.

KMKM yataja sababu za kupoteza Kimataifa
Doumbia, Young Africans ngoma ngumu