Meneja wa Manchester United Erik ten Hag ameonyesha hasira za wazi baada ya Brighton & Hove Albion kupata ushindi dakika za nyongeza na kuifanya timu yake kuwa kwenye hatari ya kukosa kupata nafasi ya kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Kiungo wa Seagulls Alexis Mac Allister, alifonga kwa penalti katika dakika ya tisa ya muda ulioongezwa baada Luke Shaw kuunawa mpira eneo la hatari na VAR ikathibitisha ni penalti.
Kipigo cha bao 1-0 kwenye Uwanja wa Amex kilidhoofisha matarajio ya United katika nafasi nne za juu, na kuwaacha pointi nne tu juu ya Liverpool walio nafasi ya tano, pamoja na mchezo mmoja mkononi.
Hag Ten alikubali upande wake ulichangia kuanguka kwao wenyewe wakati wa mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa.
Mholanzi huyo alihisi wachezaji wake hawakuwa makini ambapo, Antony alipoteza nafasi ya dhahabu kabla ya kipa, David De Gea kuokoa mkwaju wa winga wa Albion, Kaoru Mitoma kufuatia pasi mbovu kutoka kwa Victor Lindelof.
“Kila kushindwa ni jambo linaloumiza, lakini unapopoteza katika sekunde ya mwisho, bila shaka hiyo inakera sana,” amesema
“Na nadhani dakika ya kwanza inajumlisha kila kitu. Tunatengeneza nafasi nzuri, hatukuwa vizuri kiafya vya kutosha, kisha kwenye safu ya ushambuliaji baada ya kuruhusu nafasi kubwa kwa zawadi kutoka kwetu.”
“Na mwishowe, pia tulitoa bao na hiyo inakera kwa sababu ikiwa huwezi kushinda kwa sababu haujamaliza nafasi zako basi usipoteze.”
Ushindi wa Brighton ulilipiza kisasi maumivu ya penalti waliyopata kutoka kwa wapinzani wao katika Nusu Fainali ya Kombe la FA siku 11 tu zilizopita na kukamilisha mechi mbili za ligi dhidi ya United.
Ushindi wa vijana wa Roberto De Zerbi unawapandisha hadi nafasi ya sita kwenye msimamo, juu ya Tottenham na Aston Villa, na pointi nne nyuma ya Liverpool ya Jurgen Klopp walio katika nafasi ya tano.