Meneja wa klabu ya Manchester United, Erik Ten Hag amesema kuwa beki wake raia wa kimataifa wa Sweden, Victor Lindelof hauzwi na yupo kwenye mipango yake ya muda mrefu ndani ya timu hiyo.
Ten Hag yupo tayari kumwachia beki wake raia wa England, Harry Maguire lakini si Lindelof ambaye amekuwa kwenye kiwango bora hasa katika michezo ya mwishoni kitu kilichomfanya kocha kumwamini na kuhitaji kuendelea kuwa naye kikosini.
Klabu za Inter Milan (Italia) na Frankfurk (Ujerumani) ziliulizia huduma ya beki huyo katika dirisha dogo la Januari.
Lakini Man United hawakuwa tayari kumwachia beki huyo na klabu hizo zimerudi tena dirisha hili lakini kocha wa klabu hiyo hayuko tayari kumwachia.
Ten Hag yuko kwenye mpango wa kuitengeneza timu hiyo kwa muda mrefu na kuirudisha kwenye mafanikio kama miaka ya nyuma, hivyo anahitaji kubakiza wachezaji wake muhimu kwenye kikosi na moja ya wachezaji hao ni Lindelof.
Mwanzoni mwa msimu ilionekana kama Lindelof hatakuwa na muda mrefu ndani ya timu hiyo kutokana na ufinyu wa nafasi ambao alikuwa anaupata, lakini imekuwa tofauti kwani kocha alimwamini beki huyo kwa kumpa nafasi na yeye ameweza kulipa vizuri fadhila kwa kuonesha kiwango bora.