Christian Eriksen amesema Manchester United inamsajili mshambuliaji bora na mwenye nguvu kama itampata nyota wa kimataifa wa Denmark, Rasmus Hojlund.
Hojlund anajiandaa kukamilisha usajili kutua Old Trafford kutoka Atalanta baada ya makubaliano ya Pauni 72 milioni kumsajili nyota huyo wa miaka 20, kwa mkataba wa miaka mitano.
Hojlund anakamilisha vipimo vya afya ndani ya Man United kumaliza maisha ya Atalanta, huenda akaichezea timu hiyo ya kocha Erik ten Hag katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Lens kwenye Uwanja wa Old Trafford, Jumamosi (Agosti 05).
Alipoulizwa mashabiki wa Man United watarajie nini kutoka kwa Hojlund, Eriksen alisema: “Ninavyomjua? Ni mchezaji bora wa nafasi ya namba 9. Amekuwa kwa kiwango kikubwa kwa sasa.”
Mauricio Pochettino amebainisha kwamba kiungo mpya aliyesajiliwa juzi Jumapili (Julai 30), Lesley Ugochukwu ameletwa kwa ajili ya kutolewa kwanza kwa mkopo msimu huu, kwani anahitaji kiungo mzoefu.