Mchezaji wa timu ya taifa ya Denmark, Christian Eriksen anatarajiwa kupandikizwa betri ndogo maalumu ya kufuatilia mapigo yake ya moyo na kuzalisha umeme unaoendesha moyo pale itakapotakikana.

Daktari wa mchezaji huyo, Morten Boesen amethibitisha kuwa licha ya kwamba mchezaji huyo sasa anaendelea vizuri, lakini kifaa hicho kinachofahamika kwa kimombo kama ‘Cardioverter Defibrillator (ICD)’ kinatarajiwa kupachikwa maeneo ya kifuani kwake.

Wiki iliyopita mchezaji huyo alipata mshtuko wa moyo ‘cardiac arrest’ na kuanguka uwanjani akiwa anachezea timu yake ya Taifa  dhidi ya Finland katika mechi za kuwania kombe la Euro 2020.

Daktari wake alieleza kuwa mchezaji huyo ambaye pia anachezea klabu ya Inter Millan ya nchini Italia, alinusurika kupoteza maisha, iwapo asingepatiwa huduma ya kufufua moyo na mapafu viweze kufanya kazi tena yaani CPR.

Festo Sanga amshukuru Rais Samia
Ambundo anukia Jangwani