Mbunge wa Bunda Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ester Bulaya amekamatwa na jeshi la polisi Wilayani Tarime kwaajili ya mahojiano na jeshi hilo kwa kile kilichoelezwa kufanya mkutano nje ya jimbo lake.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene ambapo amethibitisha kukamtwa kwa mbunge huyo na jeshi la polisi kwa kosa la kushiriki kwenye mkutano wa Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, John Heche uliofanyika jana.
“Ester Bulaya amekamatwa leo na kufikishwa polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya, polisi wamedai kuwa walikuwa wanamtafuta baada ya yeye kushiriki kwenye mkutano wa hadhara ambao ulifanyika Nyamongo, kwenye jimbo la Tarime vijijini ambapo Mbunge John Heche alikuwa na ziara ya jimbo,”amesema Makene
-
Wabunge wa Maalim waondoka vichwa chini mahakamani
-
Lema ampigia magoti JPM, amtaka aruhusu maandamano
-
Mbowe aonya kuhusu kauli za viongozi
Hata hivyo, Mbunge huyo wiki hii alikuwa na ziara katika jimbo lake kusikiliza maoni mbalimbali ya watu na kuwashukuru wananchi wake kwa kuwa wavumilivu kwa muda mrefu kufuatia kesi mbalimbali ambazo zilikuwa zikimuandama.