Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Bunda Mjini kwa tiketi ya CCM, Stephen Wassira kupinga ushindi wa Esther Bulaya (Chadema).

Wassira alipinga vikali matokeo ya uchaguzi huo akidai kuwa uligubikwa na udanganyifu na hujuma dhidi yake ikiwa ni pamoja na kutofautiana kwa idadi ya wapiga kura kwenye kituo na jumla ya kura zilizoonekana kwenye fomu za matokeo. Wassira aliiomba mahakama kubatilisha ushindi wa Bulaya.

Bulaya alihamia Chadema akitokea CCM na kupewa nafasi ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita na hatimaye kumshinda mwanasiasa huyo mkongwe aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka mingi na waziri wa serikali ya awamu ya nne.

Kupitia Facebook, Esther Bulaya ameandika kuhusu hukumu ya kesi hiyo:

“ Wasira kwa wananchi, na leo nimemshinda kisheria, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya Uchaguzi dhidi yangu, iliyofunguliwa na wapambe wa wasira. Mungu husimama na watu waliowema. Nakutumaini mungu wangu na wewe ndiye mlinzi wangu.Asante sana Wananchi wangu wa Bunda Mjini mliokwenda Mwanza kusikiliza Hukumu. Mbunge wenu nipo dodoma tayari kwa kuanza vikao vya Bunge Kesho.”

Viongozi Wa Man Utd Wamuongezea Kiburi Louis Van Gaal
Magufuli akiahidi anatekeleza; Ujenzi wa Flyovers waanza kwa vitendo