Mzimu wa kamatakamata ya Polisi unaendelea kuwaandama wabunge wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa ambapo jana ulimuangikia mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya.

Mbunge huyo alikamatwa jana na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza na kulazimika kulala rumande baada ya jeshi hilo kumnyima dhamana kwa sababu ambazo hawakuzeweka wazi.

Taarifa kutoka jijini humo zimeeleza kuwa kikosi cha Jeshi la Polisi kilivamia katika hotel aliyofikia mbunge huyo majira ya saa saba usiku na kumkamata mbunge huyo. Bulaya alifikishwa katika kituo cha Polisi akiwa ameambatana wabunge wenzake Halima Mdee, Joyce Sokombe pamoja na mwanasheria wa John Mallya.

Mbunge huyo amekamatwa kutokana na amri ya Bunge, baada ya kushindwa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Maadili.

Haikufahamika mara moja sababu za jeshi hilo kumkamata mbunge huyo machachari aliyehamia Chadema akitokea CCM mwaka jana.

Viongozi wa Chadema pamoja na wabunge wote wa chama hicho leo wamekutana jijini humo kwa ajili ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho chenye lengo la kumpata Katibu Mkuu.

Mkurugenzi wa Jiji Dar ni Jipu linaloonewa haya?
Lowassa amzungumzia Katibu Mkuu mpya wa Chadema