Mkuu wa majeshi nchini Ethiopia ameuawa kwa kupigwa risasi katika jaribio la kutaka kuipindua serikali iliyopo madarakani.
Katika jaribio hilo ambalo limeongozwa na kiongozi wa usalama wa eneo la Amhara, limesanabisha vifo vya viongozi wa ngazi za juu wakiwemo, mkuu wa majeshi, Rais wa mkoa wa Amhara na mshauri mkuu wa Amhara.
Mkuu huyo wa majeshi, Seare Mekonnen alipigwa risasi na mlinzi wake wakati alipokuwa akijaribu kuzuia watu wenye silaha ambao walikuwa wamevamia kikao huko Addis Ababa.
Waziri mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed, ndiye aliyetoa taarifa ya kutokea kwa jaribio hilo la mapinduzi na kuuawa kwa mkuu wa majeshi leo asubuhi ambapo amesema kuwa “Mkuu wa majeshi amepigwa risasi na watu wake wa karibu”
Baada ya jaribio hilo la mapinduzi hadi sasa huduma ya ‘inaneti’ bado haipatikani nchini humo, huku Marekani ikiwa imewatahadharisha wafanyakazi wake mjini Addis Ababa kutotoka nje, ikisema kuwa ina taarifa kuhusu mashambulizi ya risasi siku ya jumamosi.
Tangu uchaguzi wa mwaka jana Waziri mkuu Abiy amekua akipambana kumaliza mvutano wa kisiasa kwa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, kuondoa vikwazo dhidi ya vyama vya kisiasa na kuwashtaki maafisa wanotuhumiwa kukiuka haki za binadamu.