Abiye Ahmed ambaye ni raia kutoka jamii ya Oromo inayoongoza kuwa na watu wengi Ethiopia, amechaguliwa kuwa waziri mkuu mpya nchini humo kufuatia kujiuzulu kwa Hailemariam Desalegn mwezi uliopita.

Ahmed alichaguliwa kwa kura zaidi ya asilimia 60 ambazo zilipitishwa na viongozi 180 wa chama cha  Ethiopian People’s Revolutionary Democratic Front (EPRDF), na kumchagua kuwa mwenyekiti wa chama hicho ambaye amepewa dhamana ya kukiongoza.

Taifa hilo kwa sasa liko katika hali ya dharura iliyotangazwa kwa ajili ya kumaliza maandamano ya takriban miaka mitatu dhidi ya serikali.

Dkt Ahmed, 42, ametazamwa na wengi kama mwenye kuzungumza kwa uwazi, mwenye ujuzi na uzoefu, na mwenye kukumbatia uongozi wa kuwashirikisha wote.

Anaaminika kuwa na ufuasi mkubwa miongoni mwa vijana wa Kioromo na pia katika jamii nyingine.

Ahmed amechaguliwa baada ya mkutano wa siku kadhaa uliofanywa na viongozi wa muungano tawala wa Ethiopian People’s Revolutionary Democratic Front (EPRDF).

Aidha Ethiopia imeanza harakati za maandamano ya kuipinga serikali yao mnamo mwaka 2015 wakipinga dhidi ya haki za umiliki wa ardhi siasa na haki za binadamu.

 

 

Uganda yavifungia vituo vya redio 23.
Kikwete kuongoza harambee ya bilioni 1, Lindi