Uongozi wa klabu bingwa nchini England Manchester City, umeanza mpango wa kuwashirikisha mashabiki kuhusu hatma ya upanuzi wa uwanja wa Etihad, ili uweze kuchukua mashabiki wengi kwa wakati mmoja.
Uongozi wa klabu hiyo ya mjini Manchester, umedhamiria kufanya hivyo baada ya kuona asilimia kadhaa mashabiki wamekua wakikosa nafasi ya kuishuhudia timu yao pindi inapocheza michezo yake ya nyumbani.
Mpango uliopo kwa uongozi wa Man City ni kutanua jukwaa la kaskazini la uwanja wa Etihad kwa kuongeza viti, ambapo utaufanya uwanja huo kuwa na viti vya mashabiki 63,000 kutoka viti 55,000.
Wazo wa kutanua uwanja wa Etihadi upande wa mashabiki lilianza kuchukua nafasi tangu mwaka 2014, lakini lililazimika na kuwekwa kando na uongozi wa klabu hiyo ambao ulihitaji kujiridhisha ni upande gani sahihi wa kuufanyia ongezeko hilo.
Kwa sasa mashabiki wa Man City wameanza kuhusishwa kwa kuwasilishiwa maswali maalum (questionnaire), ambayo yatatoa picha kamili ya mradi huo kuendelea ama kusitishwa.
Pendekezo lingine la maboresho ya uwanja wa Etihad lililodhamiriwa na uongozi, ni kuongeza zahati mbili pamoja na sehemu ya vinywaji kwa mashabiki (BAR).