Mkongwe wa soka kutoka Cameroon, Samuel Eto’o ametia nanga katika safari yake ya soka baada ya kucheza kwa miaka 23 mfululizo.

Eto’o ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 38 baada ya kuanza safari yake ya soka barani Ulaya mwaka 1996 alipotua katika klabu ya Real Madrid.

Katika miaka yake 23 kwenye soka, amevitumikia vilabu 13 tofauti ndani ya mataifa sita tofauti, ambapo anastaafu akiwa nchini Qatar katika klabu ya Qatar Sc.

Yeye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON hadi sasa na ndiye mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya RCD Mallorca.

Katika klabu alizopita alifanikisha timu zake kupata makombe 18 ambapo matatu ya Laliga, mawili ya Copa Del Rey, mawili ya Supercopa de Espana, matatu ya UEFA champions league, mawili ya Coppa Italia, mawili ya African cup on Nations AFCON, moja la Serie A, moja la Supercoppa Italiana, moja la FIFA club Word Cup, na Olympic Gold Medal.

Na kwa upande wa mafanikio yake binafsi katika soka amefanikiwa kupata medali sita ambazo ni medali ya mchezaji bora wa mwaka Afrika mara nne, mchezaji bora kijana wa mwaka Afrika mara moja, Mfungaji bora a michuano ya AFCON mara mbili, mshambuliaji bora wa UEFA wa mwaka mara moja na mpira wa dhahabu katika kombe la dunia mara moja.

Jogoo Maurice ashinda kesi mahakamani
Sudan yarudishiwa uanachama AU