Umoja wa Ulaya umechukua hatua za kisheria dhidi ya Uingereza, kufuatia mipango ya nchi hiyo ya kutunga sheria itakayokiuka sehemu ya mkataba wa Brexit uliotiwa saini mwaka uliopita.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema mpango huo wa Uingereza ni ukiukaji wa wazi wa nia njema iliyoahidiwa na kila upande katika makubaliano ya nchi hiyo kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya, Brexit.

Von der Leyen amesema iwapo muswada huo tata kuhusu soko la ndani la Uingereza utaidhinishwa utazusha mgawanyiko kwenye itifaki kuhusu Ireland Kaskazini na Kusini, iliyoafikiwa katika mkataba wa Brexit.

Umoja wa Ulaya una wasiwasi kuwa sheria hiyo inaweza kurejesha vikwazo vya kibiashara na uhamiaji kwenye mpaka kati ya Ireland Kaskazini iliyo sehemu ya Uingereza, na Jamhuri ya Ireland iliyo mwanachama wa kanda ya Ulaya.

Yanga: Mkataba wa Morrison na Simba ni batili!
Tanzania isamehewe madeni - HDT