Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu amekiri kuwepo kwa sintofahamu ya hapa na pale ya mahusiano baina ya Umoja wa Ulaya na Tanzania katika miaka mitatu nyuma iliyopita, ambapo kwa sasa mahusiano hayo yametengemaa na milango kufunguliwa.

Rais Samia amyasema hayo katika mahojiano ya kipindi maalum na Idhaa ya kiswahili Deutsche Well alipokuwa akijibu swali la mtangagazi wa kituo hicho la mahusiano ya Tanzania na Umoja wa Ulaya yakoje.

Amesema kuwa kipindi cha mahusiano kutokuwa vizuri EU Ilizuia kiasi cha fedha Euro millioni 111.5 kilichokuwa kimebaki katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya mpango wa miaka mitano iliyopita ambapo baadhi ya fedha zilitumika.

“Mpaka wakati wanafunga tulikuwa tunatekeleza mpango wa miaka mitano iliyopita ambapo Tanzania ilishatumia fedha kiasi lakini ilibaki euro million 111.5 ambazo hazikutumika mpango uliopita na zile zilikuwa za mwaka 2021 kwa hiyo sasa hivi tumekubaliana wamezifungua, tayari tumesha saini zitatoka,”. Amesema Rais Samia.

Sambamba na hayo yote Rais Samia amesema kuwa Tanzania imesaini mikataba mingine ya kimaendeleo ambapo fedha zimeshawekwa.

Uandikishwaji wanafunzi wa awali wafikia 92%
Kuelekea uchaguzi Mkuu Kenya:Ruto kinara akifuatiwa na Raila