Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila amesema kuwa ataendelea kushiriki katika siasa nchini humo hata baada ya kuondoka madarakani baada ya uchaguzi utakaofanyika wiki mbili zijazo.
Hayo yanajiri huku Umoja wa Ulaya ukitangaza kwamba umeongeza muda wa kutekelezwa kwa vikwazo dhidi ya watu 14 mashuhuri nchini DR Congo hadi Desemba mwaka ujao.
Aidha, miongoni mwa wanaoathiriwa na vikwazo hivyo ni mgombea wa muungano wa rais Kabila, Emmanuel Ramazani Shadary.
Watu hao walikuwa wamewekewa vikwazo vya kuzuiliwa kwa mali zao na pia kupigwa marufuku ya kutoingia Umoja wa Ulaya kutokana na juhudi za kuhujumu mchakato wa uchaguzi nchini DRC na ukiukaji wa haki za kibinadamu.
Hata hivyo, kwa muda mrefu, ilikuwa bado haijabainika iwapo Rais Kabila, angewania tena hadi alipoamua kumtangaza Shadary kuwa mgombea wa muungano wake wa kisiasa.
-
Mgogoro wa Burundi na Rwanda wazidi kufukuta
-
Mfahamu Wilhelm Bleek aliye linganisha sarufi za Kibantu na kuziunganisha
-
Mbaroni kwa kumhonga RC majani ya chai ya kichina